Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 2:2 - Swahili Revised Union Version

Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wafalme wa dunia wanajitayarisha; watawala wanashauriana pamoja, dhidi ya Mwenyezi-Mungu na mteule wake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wafalme wa dunia wanajitayarisha; watawala wanashauriana pamoja, dhidi ya Mwenyezi-Mungu na mteule wake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wafalme wa dunia wanajitayarisha; watawala wanashauriana pamoja, dhidi ya Mwenyezi-Mungu na mteule wake.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya dhidi ya Mwenyezi Mungu na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 2:2
27 Marejeleo ya Msalaba  

Bwana yu mkono wako wa kulia; Atawaponda wafalme, Siku ya ghadhabu yake.


Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima, Enyi watawala wa dunia, mwaonywa.


Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.


Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walikuja wote pamoja.


Mara Walipouona, wakashtuka; Wakafadhaika na kukimbia.


Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.


Usiisahau sauti ya watesi wako, Ghasia yao wanaokupinga inapaa daima.


Hema za Edomu, na Waishmaeli, Na Moabu, na Wahagari,


Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.


na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa BWANA; kwa kuwa yeye husikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia BWANA; na sisi tu nani, hata mkatunung'unikia?


Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.


Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.


Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi.


Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;


Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;


Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;


Saa ile ile Mafarisayo kadhaa walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.


Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).


Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.


habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.


Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa?


Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.