Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.
Yoshua 21:11 - Swahili Revised Union Version Nao wakawapa Kiriath-arba, ndio Hebroni, (huyo Arba alikuwa baba yake Anaki), katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na mbuga zake za malisho yaliyouzunguka pande zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipewa Kiriath-arba yaani Hebroni (Arba alikuwa baba yake Anaki) katika milima ya Yuda, pamoja na mbuga zilizoizunguka. Biblia Habari Njema - BHND Walipewa Kiriath-arba yaani Hebroni (Arba alikuwa baba yake Anaki) katika milima ya Yuda, pamoja na mbuga zilizoizunguka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipewa Kiriath-arba yaani Hebroni (Arba alikuwa baba yake Anaki) katika milima ya Yuda, pamoja na mbuga zilizoizunguka. Neno: Bibilia Takatifu Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na eneo lake la malisho lililouzunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.) Neno: Maandiko Matakatifu Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.) BIBLIA KISWAHILI Nao wakawapa Kiriath-arba, ndio Hebroni, (huyo Arba alikuwa baba yake Anaki), katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na mbuga zake za malisho yaliyouzunguka pande zote. |
Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.
Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka.
Hata ikawa mwisho wa miaka minne, Absalomu akamwambia mfalme, Tafadhali uniache niende nikaondoe nadhiri yangu, niliyomwekea BWANA huko Hebroni.
Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hadi katika nchi yenye milima kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yudea,
Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriath-arba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao Waanaki. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.
nayo ilikuwa kwa ajili ya wana wa Haruni, wa jamaa ya Wakohathi, waliokuwa wa wana wa Lawi; kwa kuwa kura ya kwanza ilikuwa ni yao.
Lakini mashamba ya mji, na vile vijiji vyake, wakampa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.
Kisha Yuda akawafuatia hao Wakanaani waliokaa katika Hebroni; (jina la Hebroni hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-arba;) nao wakamwua Sheshai, na Ahimani, na Talmai.
na kwa hao wa Hebroni, na kwa hao wa kila mahali alipotembelea Daudi mwenyewe na watu wake.