Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 14:15 - Swahili Revised Union Version

15 Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriath-arba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao Waanaki. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Mji wa Hebroni hapo awali uliitwa Kiriath-arba. Arba alikuwa mtu maarufu kuliko wote kati ya Waanaki. Nchi nzima ikawa tulivu bila vita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Mji wa Hebroni hapo awali uliitwa Kiriath-arba. Arba alikuwa mtu maarufu kuliko wote kati ya Waanaki. Nchi nzima ikawa tulivu bila vita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Mji wa Hebroni hapo awali uliitwa Kiriath-arba. Arba alikuwa mtu maarufu kuliko wote kati ya Waanaki. Nchi nzima ikawa tulivu bila vita.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 (Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kuitanishwa na Arba aliyekuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.) Kisha nchi ikawa na amani bila vita.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 (Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kutokana na huyo Arba ambaye alikuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.) Kisha nchi ikawa na amani bila vita.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriath-arba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao Waanaki. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.

Tazama sura Nakili




Yoshua 14:15
16 Marejeleo ya Msalaba  

Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.


Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka.


Akamwambia, Nenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akamtuma kutoka bonde la Hebroni, na akafika Shekemu.


Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua;


Na kuhusu habari za vijiji na mashamba yake; wengine wa wana wa Yuda walikuwa wakikaa Kiriath-arba na vijiji vyake, na katika Diboni na vijiji vyake, na Yekabzeeli na vijiji vyake;


Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa makabila yao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.


Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi hata hivi leo, kwa sababu, alikuwa mwaminifu kwa BWANA, Mungu wa Israeli.


Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, Kiriath-arba, ndiyo Hebroni (ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki).


Nao wakawapa Kiriath-arba, ndio Hebroni, (huyo Arba alikuwa baba yake Anaki), katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na mbuga zake za malisho yaliyouzunguka pande zote.


Lakini mashamba ya mji, na vile vijiji vyake, wakampa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.


Kisha wakampa huyo Kalebu Hebroni, kama alivyonena Musa naye akawafukuza wale wana watatu wa Anaki.


Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka arubaini. Kisha Othnieli, mwana wa Kenazi, akafa.


Basi Moabu alishindwa siku hiyo chini ya mikono ya Israeli. Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka themanini.


Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arubaini.


Ndipo Midiani walishindwa mbele ya wana wa Israeli, wala hawakuinua vichwa vyao tena. Nayo nchi ilipata kuwa na amani muda wa miaka arubaini katika siku za Gideoni.


na kwa hao wa Hebroni, na kwa hao wa kila mahali alipotembelea Daudi mwenyewe na watu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo