Yohana 20:14 - Swahili Revised Union Version Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kusema hayo, aligeuka nyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitambue ya kuwa ni Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kusema hayo, aligeuka nyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitambue ya kuwa ni Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kusema hayo, aligeuka nyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitambue ya kuwa ni Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Isa amesimama, lakini hakumtambua. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Isa amesimama, lakini hakumtambua. BIBLIA KISWAHILI Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. |
Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
Baada ya hayo akawatokea wawili miongoni mwao, akiwa na sura nyingine; nao walikuwa wakitembea njiani kwenda mashambani.
Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye alikuwa amemtoa pepo saba.