Yohana 19:1 - Swahili Revised Union Version Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Pilato akaamuru Yesu achukuliwe, apigwe viboko. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Pilato akaamuru Yesu achukuliwe, apigwe viboko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Pilato akaamuru Yesu achukuliwe, apigwe viboko. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Pilato akamtoa Isa akaamuru apigwe mijeledi. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Pilato akamtoa Isa akaamuru apigwe mijeledi. BIBLIA KISWAHILI Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. |
Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
kisha watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulubisha; na siku ya tatu atafufuka.
Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa minyororo, na kwa kutiwa gerezani;
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.