Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 50:6 - Swahili Revised Union Version

6 Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mgongo wangu niliwaachia walionipiga, mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu; walioniaibisha na kunitemea mate, sikujificha mbali nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mgongo wangu niliwaachia walionipiga, mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu; walioniaibisha na kunitemea mate, sikujificha mbali nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mgongo wangu niliwaachia walionipiga, mashavu yangu waliozing'oa ndevu zangu; walioniaibisha na kunitemea mate, sikujificha mbali nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao, mashavu yangu wale wang’oao ndevu zangu; sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha na kutemewa mate.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao, mashavu yangu wale wang’oao ndevu zangu; sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha na kutemewa mate.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.

Tazama sura Nakili




Isaya 50:6
20 Marejeleo ya Msalaba  

Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.


Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.


Wao hunichukia, na kujitenga nami, Hawaachi kunitemea mate usoni.


Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao.


Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu.


Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na asiyetambuliwa na wana wa mama yangu.


Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.


Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.


Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake; Ashibishwe mashutumu.


Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.


BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.


Ndipo wakamtemea mate usoni, wakampiga ngumi; na wengine wakampiga makofi,


Ndipo akawafungulia Baraba; na baada ya kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa ili asulubiwe.


Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampigapiga kichwani.


Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.


Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakamchukua wakampiga makofi.


Wakampiga mwanzi wa kichwa, wakamtemea mate, wakapiga magoti, wakamsujudia.


Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?


tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo