Na sasa, Ee Bwana MUNGU, wewe ndiwe Mungu, na maneno yako ndiyo kweli, nawe umemwahidia mtumishi wako jambo hili jema
Yohana 17:17 - Swahili Revised Union Version Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waweke wakfu katika ukweli; neno lako ni ukweli. Biblia Habari Njema - BHND Waweke wakfu katika ukweli; neno lako ni ukweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waweke wakfu katika ukweli; neno lako ni ukweli. Neno: Bibilia Takatifu Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndilo kweli. Neno: Maandiko Matakatifu Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli. BIBLIA KISWAHILI Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. |
Na sasa, Ee Bwana MUNGU, wewe ndiwe Mungu, na maneno yako ndiyo kweli, nawe umemwahidia mtumishi wako jambo hili jema
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.
Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Abrahamu hakufanya hivyo.
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
ikiwa kwa hakika mlisikia habari zake na kufundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu,
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.