Yohana 11:53 - Swahili Revised Union Version Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi walifanya mipango ya kumwua Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi walifanya mipango ya kumwua Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi walifanya mipango ya kumwua Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Isa. BIBLIA KISWAHILI Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua. |
Ndipo nikawashuhudia, nikawaambia, Mbona mnalala nje ya mji? Mkitenda hivi tena, nitawakamata. Tangu wakati ule hawakuja tena siku ya sabato.
Ikawa tokea wakati huo, nusu ya watumishi wangu walitumika katika kazi hiyo, na nusu yao wakaishika mikuki, na ngao, na pinde, na darii; na viongozi walikuwa nyuma ya nyumba yote ya Yuda.
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Maana nimesikia wengi wakinong'onezana; Hofu katika pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walipanga kunitoa uhai wangu.
Basi Yeremia akamwambia Sedekia, Kama nikikufunulia neno hilo, je! Hutaniua wewe? Tena, mimi nikikupa ushauri wewe hutanisikiliza.
Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari.
Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu yeyote tangu siku ile kumwuliza neno tena.
Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;
Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.
Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza.
Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.
Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua.