Yakobo 4:16 - Swahili Revised Union Version Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya. Biblia Habari Njema - BHND Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya. Neno: Bibilia Takatifu Ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kote kwa namna hii ni uovu. Neno: Maandiko Matakatifu Kama ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kwa namna hiyo ni uovu. BIBLIA KISWAHILI Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. |
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.
Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.
Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.