Yakobo 1:11 - Swahili Revised Union Version Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake. Biblia Habari Njema - BHND Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana jua kali huchomoza na kuyakausha majani ya mmea, nalo ua lake linaanguka, na uzuri wake unaharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana jua kali lenye kuchoma huchomoza na kuliunguza, likayakausha majani, na ua lake likapukutika, nao uzuri wake huharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake. BIBLIA KISWAHILI Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake. |
Kweli, watu wote hupita kama kivuli; Wao hujisumbua bure tu; Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.
Alivyotoka tumboni mwa mamaye, atakwenda tena tuputupu kama alivyokuja; asichume kitu chochote kwa ajili ya kazi yake, hata akichukue mkononi mwake.
Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!
na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa joto, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.
Hawataona njaa, wala hawataona kiu; joto halitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.
wakisema, Hao wa mwisho wamefanya kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na joto la mchana kutwa.
Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.
tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.