Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 102:4 - Swahili Revised Union Version

4 Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nimepondwa moyoni kama nyasi na kunyauka; sina hata hamu ya chakula.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nimepondwa moyoni kama nyasi na kunyauka; sina hata hamu ya chakula.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nimepondwa moyoni kama nyasi na kunyauka; sina hata hamu ya chakula.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani; ninasahau kula chakula changu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani, ninasahau kula chakula changu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 102:4
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wazee wa nyumba yake wakaondoka, wakasimama karibu naye, ili wamwinue kutoka chini; lakini hakukubali, wala hakula chakula pamoja nao.


Kisha Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu, akaingia katika chumba cha Yehohanani, mwana wa Eliashibu; hata, alipofika huko, hakula mkate, wala hakunywa maji; kwa maana alilia kwa sababu ya kosa lile la watu wa uhamisho.


Nayachukia maisha yangu; Nitayasema malalamiko yangu wazi; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.


Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka, Na mifupa yangu imeteketea kwa joto.


Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.


Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.


Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, Nami ninanyauka kama majani.


Maana ninakula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi.


Maana kama majani watakatika mara, Kama miche mibichi watanyauka.


Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka, Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.


Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.


Nilipotaka kumkumbuka Mungu nilifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.


Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.


Amenichoma viuno Kwa mishale ya podo lake.


Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu.


Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo