Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;
Waebrania 7:22 - Swahili Revised Union Version basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Biblia Habari Njema - BHND Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Neno: Bibilia Takatifu Kwa ajili ya kiapo hiki, Isa amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa ajili ya kiapo hiki, Isa amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. BIBLIA KISWAHILI basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. |
Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;
Kwa maana mtumwa wako alijifanya mdhamini wa huyu kijana kwa baba yangu, nikisema, Nisipomrudisha kwako, nitakuwa na hatia kwa baba yangu daima.
Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa kiko karibu kutoweka.