Wanaandaa meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta.
Nahumu 2:5 - Swahili Revised Union Version Awakumbuka watu wake wenye heshima; Wanajikwaa katika mwendo wao; Wanafanya haraka waende ukutani; Nacho kitu cha kuwafunika kimetayarishwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa anawaita maofisa wake, nao wanajikwaa wanapomwendea; wanakwenda ukutani himahima kutayarisha kizuizi. Biblia Habari Njema - BHND Sasa anawaita maofisa wake, nao wanajikwaa wanapomwendea; wanakwenda ukutani himahima kutayarisha kizuizi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa anawaita maofisa wake, nao wanajikwaa wanapomwendea; wanakwenda ukutani himahima kutayarisha kizuizi. Neno: Bibilia Takatifu Anaita vikosi vilivyochaguliwa, lakini bado wanajikwaa njiani. Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji, ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa. Neno: Maandiko Matakatifu Anaita vikosi vilivyochaguliwa, lakini bado wanajikwaa njiani. Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji, ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa. BIBLIA KISWAHILI Awakumbuka watu wake wenye heshima; Wanajikwaa katika mwendo wao; Wanafanya haraka waende ukutani; Nacho kitu cha kuwafunika kimetayarishwa. |
Wanaandaa meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta.
Miongoni mwao hakuna achokaye wala kukwaa; Hakuna asinziaye wala kulala usingizi; Wala mshipi wa viuno vyao hautalegea. Wala ukanda wa viatu vyao hautakatika;
Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja.
Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya.
mpanda farasi akipanda, na upanga ukimetameta, na mkuki ukimeremeta; na wingi wa waliouawa, na rundo kubwa la mizoga; mizoga isiyo na mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao.
Farasi wao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwamwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.