Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mke wa mtu.
Mwanzo 41:1 - Swahili Revised Union Version Ikawa, baada ya miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya miaka miwili mizima, Farao aliota ndoto: Alijikuta amesimama kando ya mto Nili, Biblia Habari Njema - BHND Baada ya miaka miwili mizima, Farao aliota ndoto: Alijikuta amesimama kando ya mto Nili, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya miaka miwili mizima, Farao aliota ndoto: alijikuta amesimama kando ya mto Nili, Neno: Bibilia Takatifu Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto. Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, BIBLIA KISWAHILI Ikawa, baada ya miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. |
Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mke wa mtu.
Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.
Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja.
Basi akakimbia yeye na yote aliyokuwa nayo; akaondoka akauvuka mto, na kuelekea kwenye nchi ya milima ya Gileadi.
Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani.
Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha kumbukumbu nacho kikasomwa mbele ya mfalme.
Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake wote, akisema, Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto wa kike mtamhifadhi hai.
Kisha itakuwa wasipoamini hata ishara hizo mbili, wala kuisikiliza sauti yako, basi, yatwae maji ya mtoni uyamwage juu ya nchi kavu, na yale maji uyatwaayo mtoni yatakuwa damu juu ya nchi kavu.
nena, useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto wangu ni wangu mwenyewe, nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi yangu.
Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya.
Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.
Kwa kuwa nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinyunyizia maji kwa mguu wako, kama shamba la mboga;