Mwanzo 21:21 - Swahili Revised Union Version Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alikuwa akikaa katika nyika za Parani, na mama yake akamwoza mke kutoka nchi ya Misri. Biblia Habari Njema - BHND Alikuwa akikaa katika nyika za Parani, na mama yake akamwoza mke kutoka nchi ya Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alikuwa akikaa katika nyika za Parani, na mama yake akamwoza mke kutoka nchi ya Misri. Neno: Bibilia Takatifu Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akamtwalia mke kutoka Misri. Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri. BIBLIA KISWAHILI Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri. |
Kwa hiyo, baada ya Abramu kukaa miaka kumi katika nchi ya Kanaani, Sarai mkewe Abramu alimtwaa Hajiri Mmisri, mjakazi wake, akampa Abramu mumewe, kama mke.
Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote.
Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidi nini?
Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akaamuru apewe vyakula, akampa mashamba.
oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Wana wa Israeli wakasafiri kwenda mbele, kwa safari zao kutoka jangwa la Sinai; na hilo wingu likakaa katika jangwa la Parani.
Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonesha matunda ya nchi.
Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na BWANA; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli.
Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.
Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemuona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mniruhusu, nimuoe.
Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.