Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 25:1 - Swahili Revised Union Version

1 Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Sasa, Samueli alifariki; nao Waisraeli wote wakakusanyika ili kumwombolezea. Wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akaenda zake kwenye nyika za Parani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Sasa, Samueli alifariki; nao Waisraeli wote wakakusanyika ili kumwombolezea. Wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akaenda zake kwenye nyika za Parani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Sasa, Samueli alifariki; nao Waisraeli wote wakakusanyika ili kumwombolezea. Wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akaenda zake kwenye nyika za Parani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi Samweli akafa, nao Waisraeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akateremka kwenye Jangwa la Parani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi Samweli akafa, nao Israeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akateremka kwenye Jangwa la Maoni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 25:1
20 Marejeleo ya Msalaba  

na Wahori katika mlima wao Seiri, mpaka Elparani iliyo karibu na jangwa.


Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.


Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.


Nao waliokaa katika nchi, wale Wakanaani, walipoyaona matanga katika sakafu ya Atadi, wakasema, Matanga haya ya Wamisri ni makuu kwa hiyo mahali pale paliitwa Abel-Misri, iliyo ng'ambo ya Yordani.


Ndipo Benaya, mwana wa Yehoyada, akapanda, akampiga, akamwua; naye akazikwa katika nyumba yake mwenyewe iliyoko nyikani.


Manase akalala na babaze, akazikwa katika bustani ya nyumba yake mwenyewe, yaani, bustani ya Uza. Na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.


Basi Manase akalala na babaze, wakamzika nyumbani mwake; na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.


Ole wangu mimi! Kwa kuwa ni mgeni katika Mesheki; Na kufanya makao yangu Katikati ya hema za Kedari.


Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;


Je, Baba zenu wako wapi? Je, manabii nao wanaishi milele?


Wana wa Israeli wakasafiri kwenda mbele, kwa safari zao kutoka jangwa la Sinai; na hilo wingu likakaa katika jangwa la Parani.


Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapiga kambi katika nyika ya Parani.


Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonesha matunda ya nchi.


Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na BWANA; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli.


Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolezea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolezea.


Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.


Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha.


Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaomba mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.


Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Waisraeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi.


Kisha alikuwa akirudi Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Waisraeli; na huko akamjengea BWANA madhabahu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo