BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Mwanzo 18:1 - Swahili Revised Union Version BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa joto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu alimtokea Abrahamu penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake wakati wa joto la mchana, Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu alimtokea Abrahamu penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake wakati wa joto la mchana, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu alimtokea Abrahamu penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake wakati wa joto la mchana, Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. Neno: Maandiko Matakatifu bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. BIBLIA KISWAHILI BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa joto. |
BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.
Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; aliyekuwa akikaa karibu na mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Abrahamu alibaki amesimama mbele za BWANA.
Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.
Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka.
Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,
Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.
Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani,
Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akainua macho yake na kuangalia juu, akaona ghafla mtu mmoja, mwanamume amesimama amemkabili naye alikuwa na upanga uliofutwa mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?