Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 13:18 - Swahili Revised Union Version

18 Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kwa hiyo, Abramu akangoa hema, akaenda kukaa karibu na mialoni ya Mamre kule Hebroni; huko akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kwa hiyo, Abramu akangoa hema, akaenda kukaa karibu na mialoni ya Mamre kule Hebroni; huko akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kwa hiyo, Abramu akang'oa hema, akaenda kukaa karibu na mialoni ya Mamre kule Hebroni; huko akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni. Naye akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea bwana madhabahu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Basi Abramu akahamisha hema yake, akaja na kukaa karibu na mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 13:18
17 Marejeleo ya Msalaba  

napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia jina la BWANA hapo.


Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; aliyekuwa akikaa karibu na mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.


BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa joto.


Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.


Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.


Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko.


Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka.


Akamwambia, Nenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akamtuma kutoka bonde la Hebroni, na akafika Shekemu.


Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.


Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Niupandie mji wowote wa Yuda? BWANA akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni.


Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.


Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.


Basi, nataka wanaume waombe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.


Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.


Yoshua akambariki, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi wake.


Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, Kiriath-arba, ndiyo Hebroni (ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki).


Tufuate:

Matangazo


Matangazo