Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
Mika 6:2 - Swahili Revised Union Version Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima, sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia! Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake. Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima, sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia! Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake. Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima, sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia! Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake. Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu “Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Mwenyezi Mungu, sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ana shauri dhidi ya watu wake; anatoa mashtaka dhidi ya Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya bwana, sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. Kwa kuwa bwana ana shauri dhidi ya watu wake; anatoa mashtaka dhidi ya Israeli. BIBLIA KISWAHILI Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli. |
Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasukasuka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi;
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.
Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu.
Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema BWANA, nami nitateta na watoto wa watoto wenu.
Mshindo utafika hata mwisho wa dunia; Maana BWANA ana mashindano na mataifa, Atateta na watu wote wenye mwili; Na waovu atawatoa wauawe kwa upanga; asema BWANA.
BWANA asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema BWANA.
BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.
Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.
Basi sasa, sikieni asemavyo BWANA; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako.
Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.
naziita mbingu na nchi hivi leo kushuhudia, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.