Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:9 - Swahili Revised Union Version

9 Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema BWANA, nami nitateta na watoto wa watoto wenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mwenyezi-Mungu asema, “Kwa hiyo, mimi nitawalaumu nyinyi, na nitawalaumu wazawa wenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mwenyezi-Mungu asema, “Kwa hiyo, mimi nitawalaumu nyinyi, na nitawalaumu wazawa wenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mwenyezi-Mungu asema, “Kwa hiyo, mimi nitawalaumu nyinyi, na nitawalaumu wazawa wenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema Mwenyezi Mungu. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema bwana. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema BWANA, nami nitateta na watoto wa watoto wenu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:9
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia, ili awahukumu watu wake.


Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,


BWANA asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu.


Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.


Mbona mnataka kuteta nami? Ninyi nyote mmeniasi, asema BWANA.


Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.


Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu;


Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na aondokane na usherati wake usiwe mbele ya uso wake, na uzinzi wake usiwe kati ya matiti yake;


Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.


ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamtenga na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao.


Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo