hata BWANA akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo.
Mika 2:5 - Swahili Revised Union Version Kwa hiyo hamtakuwa na mtu atakayeitupa kamba kwa kura katika mkutano wa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo hamtagawiwa sehemu yoyote ya ardhi miongoni mwa watu wake Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo hamtagawiwa sehemu yoyote ya ardhi miongoni mwa watu wake Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo hamtagawiwa sehemu yoyote ya ardhi miongoni mwa watu wake Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo hutakuwa na yeyote katika kusanyiko la Mwenyezi Mungu wa kugawanya mashamba kwa kura. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo hutakuwa na yeyote katika kusanyiko la bwana wa kugawanya mashamba kwa kura. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo hamtakuwa na mtu atakayeitupa kamba kwa kura katika mkutano wa BWANA. |
hata BWANA akawaondoa Waisraeli wasiwe mbele zake, kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote, manabii. Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe, waende nchi ya Ashuru, hata leo.
Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;
Hawatakaa katika nchi ya BWANA; lakini Efraimu atarudi Misri, nao watakula chakula najisi katika Ashuru.
Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila;
Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa BWANA.
Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.
Haya, jichagulieni watu watatu kwa ajili ya kila kabila; nami nitawatuma, nao watainuka waende kati ya hiyo nchi, na kuiandika kama urithi wao ulivyo; kisha watanijia.