Mhubiri 10:2 - Swahili Revised Union Version Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kulia; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Moyo wa mwenye hekima humwongoza kutenda yaliyo sawa; lakini mtu mpumbavu moyo wake humpotosha. Biblia Habari Njema - BHND Moyo wa mwenye hekima humwongoza kutenda yaliyo sawa; lakini mtu mpumbavu moyo wake humpotosha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Moyo wa mwenye hekima humwongoza kutenda yaliyo sawa; lakini mtu mpumbavu moyo wake humpotosha. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume, lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume, lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto. BIBLIA KISWAHILI Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kulia; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto. |
Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Lakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa.
Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu.