Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hadi katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hadi akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
Methali 7:26 - Swahili Revised Union Version Maana amewaangusha wengi aliowajeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni wengi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana amewaangusha wanaume wengi; ni wengi mno hao aliowachinja. Biblia Habari Njema - BHND Maana amewaangusha wanaume wengi; ni wengi mno hao aliowachinja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana amewaangusha wanaume wengi; ni wengi mno hao aliowachinja. Neno: Bibilia Takatifu Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa. Neno: Maandiko Matakatifu Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa. BIBLIA KISWAHILI Maana amewaangusha wengi aliowajeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni wengi. |
Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hadi katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hadi akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu elfu ishirini na tatu.
nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na uovu walioufanya.
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.