Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.
Methali 7:1 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, yashike maneno yangu, zihifadhi kwako amri zangu. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, yashike maneno yangu, zihifadhi kwako amri zangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, yashike maneno yangu, zihifadhi kwako amri zangu. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. |
Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.
Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.
na laana ni hapo msipotii maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkapotoka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati uko karibu.
Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.