Methali 5:1 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, uzisikie akili zangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, uzisikie akili zangu; |
Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu;
Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.