Methali 4:11 - Swahili Revised Union Version Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimekufundisha njia ya hekima, nimekuongoza katika njia nyofu. Biblia Habari Njema - BHND Nimekufundisha njia ya hekima, nimekuongoza katika njia nyofu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimekufundisha njia ya hekima, nimekuongoza katika njia nyofu. Neno: Bibilia Takatifu Ninakuongoza katika njia ya hekima na kukuongoza katika mapito ya unyoofu. Neno: Maandiko Matakatifu Ninakuongoza katika njia ya hekima na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka. BIBLIA KISWAHILI Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu. |
Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Lakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akachunguza, akatunga mithali nyingi.
akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?
Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.