Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.
Methali 29:6 - Swahili Revised Union Version Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake, lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake, lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake, lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi. Neno: Bibilia Takatifu Mwovu hutegwa na dhambi yake mwenyewe, bali mwenye haki hushangilia na kufurahi. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi. BIBLIA KISWAHILI Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi. |
Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.
Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.
Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.
wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambaye amewanasa, hata wakayafanya mapenzi yake.
Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,
Ndipo watu wa Israeli wakageuka, na watu wa Benyamini walishtushwa; kwa kuwa waliona ya kwamba wamefikiwa na maafa.