Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 15:1 - Swahili Revised Union Version

1 Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Hapo, Mose pamoja na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi-Mungu wimbo huu, “Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari, farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Hapo, Mose pamoja na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi-Mungu wimbo huu, “Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari, farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Hapo, Mose pamoja na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi-Mungu wimbo huu, “Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu kwani ameshinda kwa fahari, farasi na mpandafarasi wake amewatosa baharini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ndipo Musa na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi Mungu wimbo huu: “Nitamwimbia Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ametukuzwa sana. Farasi na mpanda farasi amewatosa baharini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ndipo Musa na Waisraeli wakamwimbia bwana wimbo huu: “Nitamwimbia bwana, kwa kuwa ametukuzwa sana. Farasi na mpanda farasi amewatosa baharini.

Tazama sura Nakili




Kutoka 15:1
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe uliipasua bahari mbele yao, hata wakapita katikati ya bahari katika nchi kavu; na wale waliokuwa wakiwafuatia ukawatupa vilindini, kama jiwe katika maji makuu.


Kumbuka kuitukuza kazi yake, Watu waliyoiimbia.


Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.


Ndipo walipoyaamini maneno yake, Waliziimba sifa zake.


Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.


Na wamshukuru BWANA, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.


Kimbilio langu utanilinda nisipate mateso, Utanizungusha nyimbo za kufurahia wokovu wangu.


Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.


Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe; Naye ni nani awezaye kusimama ukasirikapo?


BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi wao.


Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji na BWANA akawaangamiza hao Wamisri katika bahari.


Miriamu akawaitikia, Mwimbieni BWANA kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.


Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa ujeuri.


Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi.


Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo.


na kwa wewe nitamvunjavunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunjavunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;


Kwa maana nitayaondoa majina ya Mabaali kinywani mwake, wala hawatatajwa tena kwa majina yao.


Walakini nitamfurahia BWANA Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.


Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu; Bubujika Ee kisima; kiimbieni;


akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuziaibisha hadharani, akiziongoza kwa ushindi wake wa shangwe.


Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo