naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.
Methali 28:8 - Swahili Revised Union Version Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini. Biblia Habari Njema - BHND Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini. Neno: Bibilia Takatifu Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini. BIBLIA KISWAHILI Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. |
naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.
Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.
Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
naye amekopesha watu ili apate faida, na kupokea ziada; je! Ataishi baada ya hayo? La, hataishi; amefanya machukizo hayo yote; hakika atakufa; damu yake itakuwa juu yake.
tena ikiwa ameuzuia mkono wake asimwonee maskini, wala hakupokea faida na ziada, naye amezifanya hukumu zangu, na kuzifuata sheria zangu; hatakufa huyu kwa sababu ya uovu wa baba yake, hakika ataishi.
ambaye hakumkopesha mtu ili apate faida, wala hakupokea ziada ya namna yoyote; naye ameuepusha mkono wake na uovu, na kufanya hukumu ya haki kati ya mtu na mwenzake;