Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitaimarishwa milele.
Methali 27:24 - Swahili Revised Union Version Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Ladumu tangu kizazi hata kizazi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana utajiri haudumu milele, wala taji haidumu vizazi vyote. Biblia Habari Njema - BHND Maana utajiri haudumu milele, wala taji haidumu vizazi vyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana utajiri haudumu milele, wala taji haidumu vizazi vyote. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nalo taji halidumu vizazi vyote. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Ladumu tangu kizazi hata kizazi? |
Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitaimarishwa milele.
Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
Kuna balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima;
Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Mwambie mfalme, na mama ya mfalme, Nyenyekeeni na kuketi chini; Kwa maana vilemba vyenu vimeshuka, naam, taji la utukufu wenu.
Bwana MUNGU asema hivi; Kiondoe kilemba, livue taji; haya hayatakuwa tena kama yalivyo; kikweze kilicho chini, kakishushe kilichoinuka.
Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru.