Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 27:23 - Swahili Revised Union Version

23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng'ombe wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Angalia vizuri hali ya mifugo yako; tunza vizuri wanyama wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Angalia vizuri hali ya mifugo yako; tunza vizuri wanyama wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Angalia vizuri hali ya mifugo yako; tunza vizuri wanyama wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi; angalia ng’ombe wako kwa makini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ng’ombe zako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng'ombe wako.

Tazama sura Nakili




Methali 27:23
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote.


Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.


Farao akazunguka na kuingia nyumbani mwake, wala hata hilo hakuliweka moyoni.


Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.


Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Niliona, nikapata mafundisho.


Lisikieni neno la BWANA, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.


Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.


Na ninyi, kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana MUNGU.


Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.


akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii.


lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.


Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo