BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
Methali 25:6 - Swahili Revised Union Version Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usijipendekeze kwa mfalme, wala usijifanye mtu mkubwa, Biblia Habari Njema - BHND Usijipendekeze kwa mfalme, wala usijifanye mtu mkubwa, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usijipendekeze kwa mfalme, wala usijifanye mtu mkubwa, Neno: Bibilia Takatifu Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu; Neno: Maandiko Matakatifu Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu; BIBLIA KISWAHILI Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu; |
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri?
Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho,
Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.
Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,
Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.