Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.
Methali 25:5 - Swahili Revised Union Version Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waondoe waovu mbele ya mfalme, na utawala wake utaimarika katika haki. Biblia Habari Njema - BHND Waondoe waovu mbele ya mfalme, na utawala wake utaimarika katika haki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waondoe waovu mbele ya mfalme, na utawala wake utaimarika katika haki. Neno: Bibilia Takatifu Ondoa waovu mbele ya mfalme, nacho kiti chake cha ufalme kitaimarishwa kupitia kwa haki. Neno: Maandiko Matakatifu Ondoa waovu mbele ya mfalme, nacho kiti chake cha enzi kitaimarishwa kwa njia ya haki. BIBLIA KISWAHILI Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki. |
Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.
Ila mfalme Sulemani atakuwa amebarikiwa, na kiti cha enzi cha Daudi kitathibitika mbele za BWANA hata milele.
Basi mfalme akamwamuru Benaya, mwana wa Yehoyada; naye akatoka, akampiga, hata akafa. Nao ufalme ukawa imara mkononi mwa Sulemani.
Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.
Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.
Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.
Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.