Methali 24:24 - Swahili Revised Union Version Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Makabila ya watu watamlaani, taifa watamchukia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayemwachilia mtu mwenye hatia, hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa. Biblia Habari Njema - BHND Anayemwachilia mtu mwenye hatia, hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayemwachilia mtu mwenye hatia, hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” makabila ya watu watamlaani, na mataifa watamkana. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” Kabila zitamlaani na mataifa yatamkana. BIBLIA KISWAHILI Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Makabila ya watu watamlaani, taifa watamchukia. |
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.
Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia yake mbaya, na kuhifadhika;