Methali 24:20 - Swahili Revised Union Version Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana mwovu hatakuwa na mema baadaye; taa ya uhai wake itazimwa. Biblia Habari Njema - BHND maana mwovu hatakuwa na mema baadaye; taa ya uhai wake itazimwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana mwovu hatakuwa na mema baadaye; taa ya uhai wake itazimwa. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana mpotovu hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa. Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika. |
Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimwa? Na msiba wao kuwajia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake?
Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.
Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotovu huanguka katika misiba.
Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.