Methali 23:21 - Swahili Revised Union Version Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini, anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara. Biblia Habari Njema - BHND maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini, anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini, anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara. Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu. |
Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi.
mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao uko katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.