Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Methali 22:3 - Swahili Revised Union Version Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mwangalifu huona hatari akajificha, lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mwangalifu huona hatari akajificha, lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mwangalifu huona hatari akajificha, lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa. BIBLIA KISWAHILI Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. |
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuiokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;