Methali 20:10 - Swahili Revised Union Version Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu, vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu, vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu, vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, Mwenyezi Mungu huchukia vyote viwili. Neno: Maandiko Matakatifu Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, bwana huchukia vyote viwili. BIBLIA KISWAHILI Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA. |
Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo.
Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.