Methali 2:14 - Swahili Revised Union Version Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotovu wa waovu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; Biblia Habari Njema - BHND watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; Neno: Bibilia Takatifu wale wanaopenda kutenda mabaya, na kufurahia upotovu wa ubaya, Neno: Maandiko Matakatifu wale wapendao kutenda mabaya na kufurahia upotovu wa ubaya, BIBLIA KISWAHILI Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotovu wa waovu; |
Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
Mpenzi wangu afanya nini nyumbani mwangu, ikiwa amefanya uasherati? Je! Nadhiri zako na nyama takatifu zitakuondolea hatia? Ufanyapo maovu, ndipo uonapo furaha.
Yeye huwatoa wote kwa ndoana yake, huwakamata katika wavu wake, na kuwakusanya katika juya lake; ndiyo sababu afurahi na kupendezwa.
Siku ile hutaaibishwa kwa matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaojigamba na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.
ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.