Methali 19:8 - Swahili Revised Union Version Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ajipatiaye hekima anaipenda nafsi yake; anayezingatia busara atastawi. Biblia Habari Njema - BHND Ajipatiaye hekima anaipenda nafsi yake; anayezingatia busara atastawi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ajipatiaye hekima anaipenda nafsi yake; anayezingatia busara atastawi. Neno: Bibilia Takatifu Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi. BIBLIA KISWAHILI Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. |
Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.
Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme uongo.