Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 22:18 - Swahili Revised Union Version

18 maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni, na kuyakariri kila wakati.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni, na kuyakariri kila wakati.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni, na kuyakariri kila wakati.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako na kuwa nayo yote tayari mdomoni mwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako.

Tazama sura Nakili




Methali 22:18
23 Marejeleo ya Msalaba  

Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu.


Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu.


Kwa midomo yangu nimezisimulia Hukumu zote za kinywa chako.


Naifurahia ahadi yako, Kama apataye mateka mengi.


Midomo yangu na itoe sifa, Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.


Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.


Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu.


Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi; Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu.


Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.


Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu.


Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;


Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe.


Neno linenwalo wakati ufaao, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.


Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.


Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.


Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako.


Sikilizeni, maana nitasema yaliyo mazuri, Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili.


Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA, Mungu wa majeshi.


Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa BWANA wa majeshi.


Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.


Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo