Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 16:20 - Swahili Revised Union Version

20 Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Anayezingatia mafundisho atafanikiwa; heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Anayezingatia mafundisho atafanikiwa; heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Anayezingatia mafundisho atafanikiwa; heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri.

Tazama sura Nakili




Methali 16:20
22 Marejeleo ya Msalaba  

Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.


Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautikisiki, wakaa milele.


Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,


Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.


Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiaye BWANA fadhili zitamzunguka.


Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumainia.


Kila anayelidharau neno hujiletea uharibifu; Bali yeye anayeiogopa amri atapewa thawabu.


Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya muasi huangamiza.


Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.


Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema.


Maana yeye anionaye mimi aona uzima, Naye atapata kibali kwa BWANA.


Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.


Nebukadneza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.


Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala halikuonekana dhara lolote mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.


Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo