Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu.
Methali 19:6 - Swahili Revised Union Version Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye zawadi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wengi hujipendekeza kwa wakuu; kila mtu hutaka kuwa rafiki ya mtu mkarimu. Biblia Habari Njema - BHND Watu wengi hujipendekeza kwa wakuu; kila mtu hutaka kuwa rafiki ya mtu mkarimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wengi hujipendekeza kwa wakuu; kila mtu hutaka kuwa rafiki ya mtu mkarimu. Neno: Bibilia Takatifu Wengi hujipendekeza kwa mtawala na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi. Neno: Maandiko Matakatifu Wengi hujipendekeza kwa mtawala na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi. BIBLIA KISWAHILI Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye zawadi. |
Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu.
Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.
Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na Benyamini; wakaondoka, wakashuka mpaka Misri, wakasimama mbele ya Yusufu.
Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa.
Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu, uvumba na manemane.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.