Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 29:26 - Swahili Revised Union Version

26 Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala, hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala, hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala, hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA

Tazama sura Nakili




Methali 29:26
18 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.


Basi Yoabu, mwana wa Seruya, akatambua ya kuwa moyo wa mfalme unamwelekea Absalomu.


Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nilikuwa mnyweshaji wa mfalme).


Nenda ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Susa, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.


BWANA, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.


Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Kulingana na haki yake.


Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza.


Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme, Na fadhili zake ni kama wingu la masika.


Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.


Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye.


Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.


Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili; Na kila mtu ni rafiki yake atoaye zawadi.


Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.


Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu.


na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?


Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo