Israeli akamwambia Yusufu, Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionesha na uzao wako pia.
Methali 17:6 - Swahili Revised Union Version Wana wa wana ndio taji la wazee, Na utukufu wa watoto ni baba zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazee huwaonea fahari wajukuu zao; watoto huwaonea fahari wazazi wao. Biblia Habari Njema - BHND Wazee huwaonea fahari wajukuu zao; watoto huwaonea fahari wazazi wao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazee huwaonea fahari wajukuu zao; watoto huwaonea fahari wazazi wao. Neno: Bibilia Takatifu Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao. Neno: Maandiko Matakatifu Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao. BIBLIA KISWAHILI Wana wa wana ndio taji la wazee, Na utukufu wa watoto ni baba zao. |
Israeli akamwambia Yusufu, Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionesha na uzao wako pia.
Yusufu akaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu; na wana wa Makiri, mwana wa Manase, walizaliwa magotini mwa Yusufu.
Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako.
Lakini kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu;
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?