Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Methali 17:7 - Swahili Revised Union Version

7 Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu; Sembuse midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Maneno mazuri si kawaida kinywani mwa mpumbavu, sembuse maneno ya uongo kinywani mwa kiongozi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Maneno mazuri si kawaida kinywani mwa mpumbavu, sembuse maneno ya uongo kinywani mwa kiongozi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Maneno mazuri si kawaida kinywani mwa mpumbavu, sembuse maneno ya uongo kinywani mwa kiongozi!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu; Sembuse midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.

Tazama sura Nakili

Methali 17:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho cha Mungu,

Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya, Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu.

Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.

Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.

Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.

Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu.

Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni.

Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.

Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.

Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.

Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo