Hushai akaendelea kusema, Unamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake.
Methali 17:12 - Swahili Revised Union Version Afadhali mtu akutwe na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Afadhali kukutana na dubu jike aliyenyanganywa watoto wake, kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake. Biblia Habari Njema - BHND Afadhali kukutana na dubu jike aliyenyanganywa watoto wake, kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Afadhali kukutana na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake, kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake. Neno: Bibilia Takatifu Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake. BIBLIA KISWAHILI Afadhali mtu akutwe na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake. |
Hushai akaendelea kusema, Unamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake.
Akatazama nyuma akawaona, akawalaani kwa jina la BWANA. Wakatoka dubu wawili wa kike mwituni, wakawararua vijana arubaini na wawili miongoni mwao.
Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.
Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.
nitawajia kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake; nami nitararua nyama ya mioyo yao; na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali atawararua.
Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi.