Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hosea 13:8 - Swahili Revised Union Version

8 nitawajia kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake; nami nitararua nyama ya mioyo yao; na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali atawararua.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Nitawarukieni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nitawararua vifua vyenu na kuwala papo hapo kama simba; nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Nitawarukieni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nitawararua vifua vyenu na kuwala papo hapo kama simba; nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Nitawarukieni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nitawararua vifua vyenu na kuwala papo hapo kama simba; nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake, nitawashambulia na kurarua vifua vyenu. Kama simba nitawala; mnyama pori atawararua vipande vipande.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake, nitawashambulia na kurarua vifua vyenu. Kama simba nitawala; mnyama pori atawararua vipande vipande.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 nitawajia kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake; nami nitararua nyama ya mioyo yao; na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali atawararua.

Tazama sura Nakili

Hosea 13:8
11 Marejeleo ya Msalaba  

Hushai akaendelea kusema, Unamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake.

Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane wa kuwaokoa.

Nguruwe wa msituni wanauharibu, Na hayawani wa kondeni wanautafuna.

Afadhali mtu akutwe na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake.

Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.

Enyi wanyama wote wa porini njoni Mle, enyi wanyama wote wa porini.

Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wamemzunguka pande zote? Nendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale.

Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.

Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila.

Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo