Methali 16:8 - Swahili Revised Union Version Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Biblia Habari Njema - BHND Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Neno: Bibilia Takatifu Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Neno: Maandiko Matakatifu Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. BIBLIA KISWAHILI Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. |
Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.
Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.
Kama kware akusanyaye makinda asiyoyaangua, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya maisha yake itamtoka, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.
Je! Hata sasa hazina za uovu zingalimo nyumbani mwa wabaya, na kipimo kilichopunguka, ambacho ni chukizo?