Na tena, mfalme akasema hivi, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenipa leo hivi mtu wa kuketi katika kiti changu cha enzi, nayo macho yangu yakiwa yanaona hayo.
Methali 15:20 - Swahili Revised Union Version Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtoto mwenye hekima humfurahisha baba yake, lakini mpumbavu humdharau mama yake. Biblia Habari Njema - BHND Mtoto mwenye hekima humfurahisha baba yake, lakini mpumbavu humdharau mama yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtoto mwenye hekima humfurahisha baba yake, lakini mpumbavu humdharau mama yake. Neno: Bibilia Takatifu Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake. Neno: Maandiko Matakatifu Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake. BIBLIA KISWAHILI Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye. |
Na tena, mfalme akasema hivi, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenipa leo hivi mtu wa kuketi katika kiti changu cha enzi, nayo macho yangu yakiwa yanaona hayo.
Basi kwa hiyo usimwachilie, kwa kuwa wewe u mtu wa akili; nawe utajua ikupasayo umtendee, na mvi zake utazishusha Ahera pamoja na damu.
Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe BWANA leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi.
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.
Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.
Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.